Diamond Platnumz - Zuwena Text

Songtext zu Zuwena


(Ayolizer)

Mhhh!! Habari gani kaka naamini unanisikia
Mimi mzima wa afya, mama Mungu anasaidia
Toka ulipotuacha mahututi anazidiwa
Bibi presha presha nae akatangulia

Bado twakuombea ulale salama pema
Japo moyoni nina dukuduku
Natamani kusema, nisemeee
Zile mali husia ulizotuhusia tuligawa salama
Zuwena zote tukampatia tusiwe ndugu lawama
Ila Zuwena kaka amebadilika sana

Yaani shem lake Bi Zuuh wa leo sio yule wa jana

Natamani ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuona (Zuwena)
Ooooh ungemuona (Zuwena)
Aaaah Zuwena (Zuwena)
Ooooh ungemuona Zuwena (Zuwena)
Zuwena oooh (Zuwena)

Mhhh! Zuwena sasa kawa chotara
Sio tena cheusi mangala
Ngozi kaichubua awe muzungu
Anavuta na sigara
Mara Boko, Mwananyamala
Anachezesha tu miamala
Kutwa anaisugua kipepe rungu tena peku bila ndala

Aaah Zuwena siku hizi anabandika kope (Zuwena)

Zuwena mipasuo kama yote (Zuwena)
Ooh Zuwena lipa shika tuondoke (Zuwena)
Aah Zuwena wanamuita cha wote, oh!, oh!
Juzi kabebwa na majirani hata hajitambui (Zuwena)
Yaani kalewa tafarani kautwika mbwi (Zuwena)

Zuwena sio tena wa ibada na dini
Sadaka chenji asaidie
Siku hizi kageuka pedeshee wa mjini
Kutunza bendi wamsifie
Na lile gari lako urithi wa babu la kulishia ng’ombe
Siku hizi kama kwato kwenye vilabu linabebea pombe
Mama Dede kitandani hawezi hata kutembea
Zuwena ameshindwa hata kuja kumuona panadol kumletea

Natamani ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuona (Zuwena)
Ooooh ungemuona (Zuwena)
Aaaah Zuwena (Zuwena)
Ooooh ungemuona Zuwena (Zuwena)
Zuwena (Zuwena)

Siku hizi kataradadi
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Anajiita J-Lo
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Eti mzungu mweusi
Anadanga anakula ndizi kwa maganda
Anatunyoosha baba
Anadanga anakula ndizi kwa maganda

Diamond Platnumz - Zuwena Songtext

zu Zuwena von Diamond Platnumz - Zuwena Lyrics Diamond Platnumz - Zuwena Text Zuwena Diamond Platnumz Zuwena Liedtext

Noch keine Übersetzung vorhanden. Musik-Video-Miniaturansicht zu Zuwena Songtext von Diamond Platnumz

Video zum Zuwena


Zuwena Songtext von Diamond Platnumz


Andere Songtexte und Deutsche Übersetzungen

von Diamond Platnumz

Beliebt Lyrics

Patrick Scott - We Need to Talk Songtext

Patrick Scott - We Need to Talk

Songtext & Übersetzung

Beliebt Neu Songtexte